395px

Nitarejea

Diamond Platnumz

Vipi mizigo umeshaweka tayari
Sijechelewa nkaachwa na gari
Basi jikaze usilie mpenzi, aah
Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi, aah

Zile taabu na njaa
Msimu mzima mavuno hakuna
Huwa nakosa raha
Pale mkikosa cha kutafuna

Roho yangu inauma
Sema ntafanya nini na pesa sina
Nakuonea na huruma
Bora niende mjini kusaka tumaa

Kama watoto wakinililia
Waambie kesho nitarejea
Wadanganye na vibagia
Waambie pipi ntawaletea

Kama watoto wakinililia
Waambie kesho nitarejea
Nawe usichoke kuvumilia
Na kila siku kuniombea

Wanajua kwamba nafsi na roho
Vitakuwa na wasiwasi
Ukumbuke na moyo
Utajawa na simanzi

Ntakapokuwa nakwenda shambani
Afu niko peke yangu honey
Ntapokuja kuwa na majirani ntaumia aah
Pale napotoka kisimani (aah)
Ama nipo na kuni kichwani (aah)
Sina wakunitua nyumbani ntaliaa

Maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo
Hata mwenzako sijawahi kufika dar huu ndo mwanzo
Vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh
We niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh

Kama watoto wakinililia
Waambie kesho nitarejea
Wadanganye na vibagia
Waambie pipi ntawaletea

Kama watoto wakinililia
Waambie kesho nitarejea
Nawe usichoke kuvumilia
Na kila siku kuniombea

Unapokwenda kama ukifika salama
Utukumbuke na sisi
Usisahau kama mkeo na wana
Umetuacha na dhiki

Vile usijali ila naomba chunga sana
Ogopa na marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama
Waambie sidanganyiki

Unapokwenda kama ukifika salama
Utukumbuke na sisi
Kumbuka mkeo na wana nyumbani
Umetuacha na dhiki ooh

Vile usijali ila naomba chunga sana
Ogopa na marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama
Waambie sidanganyiki

Ntarejea mama
Niombee nirude salama
Oh watoto wadanganye
Ihh, oh

Kama watoto wakinililia
Waambie kesho nitarejea
Wadanganye na vibagia
Waambie pipi ntawaletea

Kama watoto wakinililia
Waambie kesho nitarejea
Nawe usichoke kuvumilia
Na kila siku kuniombea

Composição: