395px

Ntampata Wapi

Diamond Platnumz

Sura yake mtaratibu mwenye macho ya aibu
Kumsahau najaribuu ila namkumbuka Sana'a
Umbo lake mahbibu kwenye maradhi alonitibu
Siri yangu ukaribu bado namumbuka Sana'a

Alionifanya silali, jua kali nitafute tukale
Lakini hata hakujali darling akatekwa na wale
Alionifanya silali jua kali nitafute tukale
Ila wala hakujali darling aah

Ntampata wapi kama yule nilompendaga sana
Ntampata wapi kama yule nanipende sana

Aii, aii nyota ah
Nyota ndo tatizo langu
Aii nyota ah
Mpaka nalia peke yangu
Aii nyota ah
Nyota ndio shida yangu
Nyota ah
Wamenizidi wenzangu

Alidanganywa na wale (wale)
Wenye pesa nyumba gari (gari)
Mi kapuku hakunijali (jaali)
Akanikimbiaa
Alidanganywa na wale (wale)
Wa mapesa nyumba gari (gari)
Mi ungaunga hakunijali (jali)
Jaali akanikimbiaa

Alionifanya silali, jua kali nitafute tukale
Lakini hata hakujali darling akatekwa na wale
Alionifanya silali jua kali nitafute tukale
Ila wala hakujali darling aah

Ntampata wapi kama yule nilompendaga sana
Ntampata wapi kama yule anipende sana

Bado ananijia ndotoni (bado)
Kila nikiamka simwoni (bado)
Bado ananijia (ni) kilala
Haki ya mungu sio masiara

The touch Clever (bado)
Hii ni sauti ya raisi (bado)
Iliomshindaga Ibilisi (bado)
Kwa mwanadamu sio rahisi (bado)
Kamwambie (bado)
Lazima ujue kutofautisha (bado)
Kati ya msalaba na jumlisha (bado)
Kuna X na kuzidisha (bado)
Nicheche (cheche)

Bado ananijia nkilala
Haki ya Mungu sio masiara

Composição: