395px

Ongeza

Diamond Platnumz

Mmh
(Ayo Lizer)

Mi kwako sikuingia miguu
Mikono hadi kichwa
Kiufupi mazima
Nikiamini wa kufa kuzikana

Yaani hoi sio nafuu
Mututi kabisa hata mashaka sina
Ukiamini
Utatengwa na Maulana

Mvumilivu hula mbivu
Nimengoja mpaka zikaoza
Naambulia maumivu
Ningali sina wa kunipoza

Sijui yangu stahimilivu
Kunyenyekea waniponza
Napambania utulivu
Mwezangu chuki unaikoza

Sikukufuta tu machozi
Ulipolia nililia na wewe
Sasa mbona wanilipa majonzi
Yaani stress mapombe mi nilewe

We ndo wangu Yesu Mkombozi
Sa mbona Petro unaniacha mwenyewe
Nikose usingizi na njozi
Ndo ufurahi okay sawa

Si unataka nitukanwe
Ongeza ongeza bado
Nidhalilike
Ongeza ongeza bado

Nikose pa kuificha sura
Ongeza ongeza bado
Marafiki wanicheke, waning'onge ada
Ongeza ongeza bado

Mmh kisichokuua hukukomaza
Ati ikiwa sikani huo msemo nakataa
Maana jua linapoangaza na sina afadhali
Mi kwangu ni mabalaa

Ooh najitahidi kumsinga mwali
Ila somo ananikataa
Ooh penzi letu si la kibatari
Anayamwaga mafuta taa

Kutwa ni vurugu ndani
Purukushani hapakaliki
Roho inaniuma yaani
Kwanini sa tunagombana sweetie

Ooh njema gani
Niambie labda nitende kipi? (Aah)
Hata pa kucheka hunnie
Ati utani unapanic

Naelewa riziki mafungu saba
Na la kwangu sita
Naelewa sikutoshi labda
Kukuridhisha

Sikukufuta tu machozi
Ulipolia nililia na wewe
Sasa mbona wanilipa majonzi
Yaani stress mapombe mi nilewe

We ndo wangu Yesu Mkombozi
Sa mbona Petro unaniacha mwenyewe
Nikose usingizi na njozi
Ndo ufurahi okay sawa

Si unataka nitukanwe
Ongeza ongeza bado
Nidhalilike
Ongeza ongeza bado

Nikose pa kuificha sura
Ongeza ongeza bado
Ndugu jamaa wanicheke, waning'onge ada
Ongeza ongeza bado

Aah nikose pa kuificha sura
Waning'onge ada

(Wasafi)

Composição: