395px

Mbali Nawe

Jay Melody

Masikini mimi
Mwenzako mimi
Naumia sana
Japo nishajua mimi
Kuwa sawa na wewe haitawezekana
Hata nikishuka chini, ndo unaniona
Mi mjinga sana
Eti umepatwa nini, mbona hapo mwanzo ulitulia aah

Na wala sio mbali, sio mbali
Tulikua karibu na malengo
Na leo kiutani, kama utani
Umeshindwa kuumaliza mwendo
Na tena haujali, haujali
Ukiondoka utaacha pengo
Hakuna cha habari, nikae mbali
Huku kuachwa bila maelezo

Mbali nawe, mbali nawe
Mbali nawe, mbali nawe
Mbali nawe, mbali nawe
Mbali nawe, mbali nawe

Au kuwa na mie hautamani
Basi niambie kosa gani
Basi niambie jinsi gani
Utakua sawa baby mmh
Nikueleze jinsi gani
Vile nimekuweka moyoni
Hata unipime kwa mizani
Nitajaa kwako honey

Mi naumwa
Siko sawa
Lako penzi ndo yangu dawa
Mi naumwa aah
Siko sawa
Lako penzi ndo yangu dawa

Na wala sio mbali, sio mbali
Tulikua karibu na malengo
Na leo kiutani, kama utani
Umeshindwa kuumaliza mwendo
Na tena haujali, haujali
Ukiondoka utaacha pengo
Hakuna cha habari, nikae mbali
Huku kuachwa bila maelezo

Mbali nawe, mbali nawe
Mbali nawe, mbali nawe
Mbali nawe, mbali nawe
Mbali nawe, mbali nawe

Composição: