exibições de letras 5

Siwema usinipe mateso ya moyo
Na sasa nimechoka kweli nasema
Siwema usinipe mateso ya moyo
Na sasa nimechoka kweli nasema

Nilidhani nimepata mpenzi wa kweli
Nakumbe nimepatikana na mambo ya ajabu
Nia na madhumuni yako nimeshavitambua siwema kaka
Siwema kaka, ah, ah, ah

Unajitapa mbele ya rafiki zako
Kwamba mimi sina la kusema mbele yako
Umeniweka kwenye kiganja mama
Unalo taka ndilo ninalofanya sababu wewe
Ni mzuri sana, siwezi kupata mwengine kama wewe
Siwema kaka, unajidang'anya

Wema wangu ndio ulioniponza
Fadhila zote, kumbe kwako ni bure
Malipo yake, kunifanya mjinga
Hayo yote, nimakosa yangu
Lakini sasa nimejifunza kutokana na makosa
Najiepusha nawe mama aaa

Nimezunguka Tanzania bara
Unguja na pemba nimefika
Nimewaona vijana wenye sifa
Wenye kujipamba waka pambika

Kwa hiyo nielewe brother
(Sibabaishwi na sura napenda tabia njema)
Sibabaishwi na sura yako
(Sibabaishwi na sura napenda tabia njema)
Usifikiri mimi rimbukeni sana
(Aah na sura napenda tabia njema)
Nilikupenda ki mapenzi
(Sibabaishwi na sura napenda tabia njema)
Ukaniona ni mimi suga mami lako
(Sibabaishwi na sura napenda tabia njema)
Tabia njema ndio silaha yako
(Sibabaishwi na sura napenda tabia njema)
Kila mtu atakupenda kaka
(Sibabaishwi na sura napenda tabia njema)


Comentários

Envie dúvidas, explicações e curiosidades sobre a letra

0 / 500

Faça parte  dessa comunidade 

Tire dúvidas sobre idiomas, interaja com outros fãs de Lady Jaydee e vá além da letra da música.

Conheça o Letras Academy

Enviar para a central de dúvidas?

Dúvidas enviadas podem receber respostas de professores e alunos da plataforma.

Fixe este conteúdo com a aula:

0 / 500

Opções de seleção