Nakupenda
Viola Karuri
Nakupenda wewe pekee roho yangu
Yakulilia kweli eh njoo kwangu
Usiku silali mie nakuwaza we
Mawazo nenda rudi yakuzingira we
Mapenzi yako kweli yanifaa mimi
Maisha bila wewe kweli sijui
Mahangaiko yangu yameania patupu
Kutoka leo nimeyapiga marufuku
Nakupenda wewe pekee
Daima mimi na wewe
You linger in my mind
Hope you're always standing by my side
Nakupenda wewe pekee
Daima mimi na wewe
I have loved you from the start
You who holds the key to my heart
Nakupenda wewe pekee roho yako
Yapendeza kweli yanivuta kwako
Upole, ufadhila na ukarimu wa moyo
Utu bila uchoyo bali upendo kibao
Waliokutangulia hawakushiki
Hata wajaribu vipi hawakuwezi
Wala sisiti kusema ubaraka kwangu
Mvumilivu bila shaka hula bivu
Nakupenda wewe pekee sina hofu
Maisha yetu pamwe kweli si mabovu
Pawe balaa, fununu, chuki na siasa
Tukiwa pamoja yote hayo sawa sawa
Bahati nzuri tunalo pendo hili
Mwenyezi Mungu naye atubariki
Tukae pamoja siku nenda siku rudi
Katika pendo hili mi na wewe mpenzi



Comentários
Envie dúvidas, explicações e curiosidades sobre a letra
Faça parte dessa comunidade
Tire dúvidas sobre idiomas, interaja com outros fãs de Viola Karuri e vá além da letra da música.
Conheça o Letras AcademyConfira nosso guia de uso para deixar comentários.
Enviar para a central de dúvidas?
Dúvidas enviadas podem receber respostas de professores e alunos da plataforma.
Fixe este conteúdo com a aula: