Ndoa (feat. Khadija Kopa, Juma Kakere & Malkia Karen)

Bright Tanzania

Wanangu vipi baba, mbona kimya baba
Uliahidi jambo, mbona kimya baba
Mambo ya ndoa umefikia wapi baba
Mambo yako ya ndoa umekwama wapi niambie

Nimezunguka dunia mzima
Dunia kiganja baba, nimeyaona mengi
Ya walimwengu wanasema
Bora uchague mpenzi, tofauti na enzi

Wanafanana kwa sura matendo baba niko hoi eeh
Unayempenda na kumwaza anamwaza meingine
Bila pesa umaarufu mwonekano baba we hung'oi eeh
Na kwa dunia ya sasa, nioe wapi pengine

Dunia hadaa hilo baba utambue
Muda unaenda hilo uzingatie
Mweke Maulana mbele mambo yatimie
Dhamira yako ya kweli, nayo ajalie

Baba ooh baba ooh, daddy ooh (baba)
Najua una hamu sana (mwana)
Ndoa ooh, ndoa ooh, ndoa ooh
Ya mi mwanao kuiona
Kaza roho, kaza roho, dua njema
Atajibu Maulana
Mke mwema aah
Atakuja tu baba

Ayee (ayee)
Ndoa eeh (nuia baba)
Sijamuona wa kuoa eeeh (utaoa mwanangu)
Ayee (ooh ayee)
Ndoa eeh (nuia baba)
Sijamuona wa kuoa eeeh

Ng'aa tena dafaradhi
Kumhalalisha mwanangu
Kwangu mimi ni heshima
Nikimwona mkwe wangu
Kudanga danga si kwema
Kwa leta laana mwanangu
Leo Ali kesho Juma
Hebu tuzao twangu

Mama wakitongoza wanataka kuvua na nguo
Ah tumejuana leo, anataka kunivua nguo eeh
Wanaume wa sasa, suruali kushuka eeh
Mama niombee kwa Mungu
Nipate mwema niweze sitirika

Leta mjukuu nimwoe, aje anikojolee
Ooh, ooh

Mama ooh, mama ooh, mama ooh
Najua una hamu sana
Ndoa ooh, ndoa oooh, ndoa oooh
Ya mi mwanao kuiona
Kaza roho, kaza roho dua njema
Atajibu Maulana
Mume mwema aaah
Atakuja tu mama

Ayee, ndoa eeh (nuia mwana aah)
Sijamuona wa kunioa eeh (ooh nuia mwana aah)
Ayee, ndoa eeh
Sijamuona wa kunioa (sijamuona wa kunioa eeh)
I say mama ma, mama, mama
Ayee, ndoa eeh
Sijamuona wa kunioa (sijamuona wa kunioa eeh)

Utampata baba ano kuridhia
Nataka nicheze eeh, mwanangu
Siku hiyo wanione eeh, mwanangu eeh
Nikate, nikate, kwa furaha yangu wee eeh


Comentários

Envie dúvidas, explicações e curiosidades sobre a letra

0 / 500

Faça parte  dessa comunidade 

Tire dúvidas sobre idiomas, interaja com outros fãs de Bright Tanzania e vá além da letra da música.

Conheça o Letras Academy

Enviar para a central de dúvidas?

Dúvidas enviadas podem receber respostas de professores e alunos da plataforma.

Fixe este conteúdo com a aula:

0 / 500

Opções de seleção